Search This Blog

Friday, September 3, 2021

Taliban wakaribia kutangaza serikali mpya Afghanistan


Duru kutoka nchini Afghanistan zimesema watawala wapya wa taifa hilo - vuguvugu la Taliban huenda wakatangaza serikali yao leo Ijumaa, huku dunia ikusubiri kwa shauku kuona iwapo utawala mpya utatimiza ahadi zao kwa Afghanistan. 
 
Tangazo hilo, ambalo vyanzo viwili vya Taliban vililiambia shirika la habari la AFP kwamba linaweza kutolewa baada ya sala ya Ijumaa, linafanyika siku kadhaa baada ya Marekani kuondoa kikamilifu wanajeshi na kuhitimisha vita vilivyodumu kwa miaka 20.
 
 Mataifa ya Magharibi yamekumbatia mkakati wa kusubiri na kuona kuhusu ushirikiano wao na kundi la Taliban kuendelea mbele, lakini kumekuwepo na ishara za kulegeza msimamo baada ya makampuni ya uhamishaji fedha ya Western Union na MoneyGram kutangaza kuanza tena kutoa huduma kuelekea taifa hilo. 
 
Qatar ilisema ilikuwa inafanya kazi kuufungua tena ubalozi wake mjini Kabul, huku China ikiripotiwa kuahidi kuacha wazi ubalozi wake na kuimarisha zaidi uhusiano na msaada wa kibinadamu. 
 
Uvumi umeenea kuhusu muundo wa serikali mpya ya Afghanistan, ingawa afisa mmoja mwandamizi alisema wiki hii kwamba wanawake wana uwezekano mdogo wa kujumlishwa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...