Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia nidhamu ya watumishi waliochini ya kwa kuhakikisha wanatenda haki na kufuata miongozo kanuni na sheria za utumishi wa umma.
Akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo Jijini Dodoma Mhe. Silinde amesema amewataka kuhakikisha wanazingatia mipaka ya madaraka na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watumishi zifuate sheria, kanuni na taratibu za utendai kazi katika utumishi wa umma na Serikali kwa ujumla.
Mhe. Silinde amesema ni wajibu wa wakurugenzi kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ameaagiza wakurugenzi hao kutatua kero za wananchi hasa walioko maeneo ya vijijini ambao wengi ni masikini kwa kuhakikisha wanapatikana kirahisi maofisini na kuondoa urasimu usio wa lazima.
Ameendelea kufafanua kuwa bado kuna maeneo fedha za Serikali zinapotea na kuingia katika mifuko ya wajanja kwa kutumia risiti za mikono, amewataka kuhakikisha wanatumia mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato
Vilevile, Amewagiza kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi za fedha za Serikali na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kulingana na thamani ya fedha zilizotumika ikilinganishwa na huduma iliyotolewa.
Mhe. Silinde qmewataka kuhakikisha wanasimamia ubunifu na uhodari katika kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia mipango ya wananchi kupitia Halmashauri zao, na kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao
Aidha, Mhe. Silinde amesema ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi vi vyema wakaongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za waalimu , vituo vya afya, vituo vya maji safi na salama.

No comments:
Post a Comment