Search This Blog

Thursday, September 9, 2021

Raisi: Iran iko wazi kuhusu shughuli za nyuklia


Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema nchi yake iko wazi kuhusu shughuli zake za nyuklia. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya rais, kiongozi huyo amemfahamisha rais wa baraza la Ulaya Charles Michel kwa njia ya simu kwamba ushirikiano wa dhati wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia IAEA ni mfano mzuri kwamba Iran inazingatia uwazi kuhusu shughuli zake za nyuklia.
 
 hata hivyo shirika la IAEA lisema kazi yake ya usimamizi nchini Iran imekwama kwa kiwango kikubwa tangu Februari 23 baada ya serikali ya Iran kusitisha baadhi ya kazi zake za ukaguzi katika mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...