Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo atamuomba Rais wa Marekani Joe Biden uungwaji mkono katika kuisaidia nchi hiyo na vifaa vya kisasa vya kijeshi.
Haya yanakuja wakati ambapo inaripotiwa kiongozi huyo ana hofu kuhusiana na shinikizo la Urusi linalozidi siku chache baada ya Marekani kujiondoa rasmi kutoka Afghanistan.
Maafisa wa serikali ya Urusi wameiambia Ukraine kwamba Afghanistan iwe funzo kwake, kwani nchi hiyo imekuwa ikitegemea nchi za Magharibi katika mapigano ya miaka saba dhidi ya Waukraine wanaotaka kujitenga ambao wanahusishwa na Urusi.
Rais Zelensky alialikwa Washington baada ya Biden kuiondolea Urusi sehemu kubwa ya vikwazo kuhusiana na mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 akisema muda umepita mno kuusitisha mradi huo.

No comments:
Post a Comment