Rais Ebrahim Raisi wa Iran amevishutumu vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa lake kwa kuviita kama nyenzo ya kivita.
Katika hotuba yake ya kwanza tangu awe rais katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, rais huyo amesema sera za nje za Marekani zimeongeza mvurugano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hotuba Rais Raisi ya Jumanne imeonekana yenye kukosoa zaidi na kujikitia katika sera za mambo ya nje za Marekani zaidi ya hotuba za mtangulizi wake mwenye siasa za wastani, Hassan Rouhani, alizozitoa katika mikutano ya Hadhara Kuu ya Umoja wa Matiafa iliyopita.
Raisi, ambaye alikula kiapo chake cha kuliongoza taifa la Iran mwezi uliopita baada ya uchaguzi, ni kiongozi wa kihafidhina na mkuu wa zamani wa mahakama anayeonekana kuwa karibu zaidi na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

No comments:
Post a Comment