Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekaribisha uamuzi wa kumwachilia rais wa zamani Jacob Zuma kwa msamaha wa matibabu.
Rais Ramaphosa alimtakia Zuma afueni ya haraka, wakati wa hotuba yake katika mkutano wa kamati kuu ya kitaifa ya chama tawala cha ANC.
“Tunakaribisha hili. Tumesikia kuwa hayuko sawa na tungependa kumtakiaafueni ya haraka kwani amerejeshwa nyumbani kwake kuwa na wapendwa wake, ”alisema.
Siku ya Jumapili, Idara ya Huduma za Magereza ilitangaza kuwa rais huyo wa zamani atatumikia kifungo cha miezi 15 iliyobaki nyumbani.
Hali ya ugonjwa wake haikuelezwa , lakini taarifa ilisema atakamilisha adhabu yake yote chini ya masharti maalum.
Kufungwa kwake jela kulisababisha maandamano makali na uporaji.

No comments:
Post a Comment