Search This Blog

Tuesday, September 28, 2021

Rais Samia ateua wajumbe watatu NEC


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wajumbe wa tatu watakaojaza nafasi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 27, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffari Haniu imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na Asina Abdillah Omar aliyemaliza muda wake Septemba 15 mwaka huu na sasa ameteuliwa kipindi cha pili kuendelea na majukumu ya NEC.

Wengine ni Magdalena Rwebangira, kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Jaji Jacob Mwambengele wa Mahakama ya Rufani. Uteuzi huo umeanza Septemba 14 mwaka huu.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...