Search This Blog

Thursday, September 9, 2021

Mwanamke aliyebadilishwa wakati anazaliwa na kupewa familia nyingine aishtaki serikali Uhispania


Mwanamke mmoja amedai fidia kutoka kwa mamlaka ya afya kaskazini mwa Uhispania baada ya kugundua kwamba alibadilishwa kimakosa wakati wa kuzaliwa na mtoto mwingine miaka 19 iliyopita, ripoti za eneo hilo zinasema.

Mwanamke huyo alichanganywa na mtoto ambaye alizaliwa siku hiyo hiyo mnamo mwaka 2002 katika hospitali moja huko Logroño, kusini mwa Bilbao.

Watoto wote wawili waliwekwa kwenye chumba cha kuatamia kabla ya kila mmoja wao kukabidhiwa mzazi asiye sahihi.

"Serikali ya mkoa imekiri mchanganyiko huo, na kulaumu kutokea kwa "makosa ya kibinadamu."

Jumanne, waziri wa afya wa serikali ya La Rioja, Sara Alba, alisema ni vigumu kuhitimisha ni nani hasa aliyefanya kosa hilo.

Alisema "haitawezekana kwa kitu kama hiki kutokea tena hii leo" kwasababu taratibu za kutambua watoto ni "salama na za kuaminika."

Kisha hicho kimeripotiwa kwanza na gazeti La Rioja, ambalo lilisema mmoja wa wanawake hao anatafuta kulipwa € 3m (£ 2.4m; $ 3.5m) kama fidia kutoka kwa wizara ya afya ya mkoa huo.

Wizara hiyo imetoa tu fidia ya € 215,000, ripoti zinasema.

Mwanamke mwingine aliyehusika amearifiwa kuhusu hali ilivyotokea lakini hajatoa malalamiko, gazeti la El País liliripoti.

Mlalamishi, ambaye hajatajwa jina, alilelewa na mwanamke ambaye aliamini ni bibi yake.

Wakati bibi alipomshtaki aliyedhaniwa kuwa baba yake kwasababu ya kutomtunza mtoto wake mnamo mwaka 2017, mahakama iliamuru kufanyika kwa uchunguzi wa vinasaba - DNA.

Hii ilithibitisha kuwa mtu huyo hakuwa baba mzazi wa mtoto huyo, na vipimo vya baadaye vilifafanua kwamba aliyedhaniwa kuwa mama yake hakuwa na uhusiano naye wa chembe za urithi.

Wakati akiwa na miaka 16, msichana huyo aliomba msaada kutoka kwa mawakili, ambao walishinikiza mamlaka ya afya kuchunguza kilichotokea wakati wa kuzaliwa kwake.

Uchunguzi ulionyesha kuwa kulikuwa na mtoto mmoja tu msichana ambaye kuna uwezekano mkubwa angeweza kubadilishwa naye.

Sasa akiwa na miaka 19, mwanamke huyo anasubiri matokeo ya uchunguzi wa DNA ili kuthibitisha utambulisho wa wazazi wake halisi wakati waendesha mashtaka wanapochunguza kesi hiyo.

Bi Alba alisema serikali ya mkoa itaheshimu mchakato wa kisheria na itawapa familia msaada wowote wanaohitaji.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...