Search This Blog

Thursday, September 2, 2021

Muingereza mwenye asili ya Kenya anyakua taji la Miss England


Rehema Muthamia, ambaye ana asili ya Kenya, amekuwa gumzo baada ya kushinda taji la Miss world England mwaka 2021, ambaye ataiwakilisha England kwenye michuano ya Miss World 2021.

Ushindi huo umemfanya kuwa Miss England 2021 sambamba na Mister England Liam Royce Ulla.

Bi. Muthamia atapeperusha Bendera ya England Miss World, tukio litakalofanyika tarehe 16 mwezi Desemba mjini San Juan, Puerto Rico

Muthamia alizaliwa England na wazazi Wakenya na kuishi maisha yake ya utoto nchini Kenya kabla ya kuhamia England, ambako anaishi na Bibi yake huko Luton Bedfordshire.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...