Search This Blog

Wednesday, September 22, 2021

Mkuu wa Wilaya Hassan Masala ametoa ushauri huu kwa watendaji wa Halmashauri namna ya kuwapanga machinga




Na Maridhia Ngemela Mwanza.

Wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga)Mkoani Mwanza wilaya ya Ilemela wamemueleza Mkuu wa Wilaya hiyo changamoto  alipokuwa katika zoezi lakuzungukia  masoko kwa lengo la kuwapa taarifa juu ya hatua za Serikali  za kutaka kuwapanga kwa utaratibu ili wafanye biashara kwa uhuru.

Baadhi ya machinga waliopata nafasi ya kuzungumza wametoa ushauri na changamoto zilizopo katika masoko ambayo wanafanyia biashara Hassan Mbogo  kutoka soko la Buzuruga amesema kuwa Serikali ujitahidi kuweka mageti ambayo yataimalisha ulinzi wa Mali zao na kuomba baadhi ya njia zifunguliwe ili kurahisisha wateja kufika na kupata bidhaa.

Zena Zakaria kutoka soko la Nyasaka senta ameiomba serikali wapelekwe soko la Nyamuge kwa lengo la kuangalia bidhaa wanazouza ili kuweza kupata wateja kwa urahisi na miundombinu iboreshwe ili kuondoka usumbufu kwa wafanya biashara na wateja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewafafanulia wamachinga Nia ya Serikali ya kufanya zoezi hilo la kuwaandaa ikiwa ni kuwapanga vizuri kuwa ni kuwapa uhuru wa kufanya biashara kwa amani bila kubughudhiwa na mtu mmoja mmoja.

Masala amesema katika zoezi hilo wafanya biashara wameelezea changamoto zao ambazo ni ukosefu wa umeme, maji na tayali kama halmashauri tumeisha weka mikakati ya kutengeneza miundombinu hiyo ndani ya wiki tatu hizi zilizobaki nimeisha elekeza wataalamu wa sekta hizo mbili waanze ukarabati haraka iwezekanavyo ili tuzitatue mapema na  mengine tutaenda tunalekebisha mambo ya msingi

mkuu wa Wilaya alipokuwa akijibu changamoto na kupokea ushauri amesema viongo,I wa masoko kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali wasimamie zoezi hilo bila upendeleo bila kuweka makundi ambayo yataleta usumbufu hapo baadae na amesisitiza wafanya biashara wote kupata maeneo hata kwa kuwapeleka masoko jirani lengo ikiwa kuwapatia maeneo ya kufanya biashara kwa uhuru.

"Sisi tunayomaelekezo ya bei elekezi za vyumba vyetu ikitokea mtu akapangisha chumba au meza kwa bei yake tutamnyanganya chumba na kukirudisha Serikalini maana kufanya hivyo ni wizi unaiibia Serikali alafu nanyie halmashauri angalieni hizi bei kuliko vyumba kufungwa kwanini msishushe bei mkapangisha watu ili tukusanye hicho kidogo kulikokufunga hivyo vyumba tunachotaka sisi ni kukusanya mapato hata kama ni kidogo tuingize maana vikikaa bila watu huo ni uharibifu nafikili unaelewa nyumba ikikaa bila watu inaharibika nafikili kupanga ni kuchagua kwahiyo mtaangalia kipi bora amesema Masala.

Amesema kila kiongozi asimamie wajibu wake katika  zoezi hilo la kuwapanga machinga kwa ushirikiano ili kulimaliza na kutekeleza agizo hilo kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Rais Samia Suluhu na Waziri mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa ili kuwapanga vizuri wafanya biashara hao na nilazima tuwawekee umeme na maji hata mkitaka kufanya biashara massa 24 ni juu yenu kikubwa tukusanye mapato ili tuendelee kufanya miundombinu mengine.

Mkuu wa Wilaya ametembelea masoko ya Kirumba,Nyasaka,kiloleli, buzuruga,sabasaba na  pansiasi ilikufahamu changamoto hususani miundombinu na kuangalia namna ya kuwapanga machinga kwa utaratibu unaotakiwa na rafiki kwa kufanya biashara zao.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...