Search This Blog

Monday, September 6, 2021

Mkuu wa misaada ya kiutu wa UN akutana na viongozi wa Taliban

 


Kundi la Taliban limeahidi kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wanaotoa misaada ya kiutu na vilevile wa usambazaji wa misaada hiyo nchini Afghanistan. 


Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema hayo kupitia taarifa baada ya kundi hilo kukutana na Mkuu wa utoaji misaada wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths. 


Griffiths amekuwa akifanya vikao kadhaa mjini Kabul na jana alikutana na viongozi wa Taliban mnamo wakati kuna kitisho cha kutokea mgogoro wa kibinadamu nchini humo chini ya uongozi mpya wa kundi lenye misimamo mikali ya kidini. 


Ripoti imeongeza kuwa kwenye mkutano wa Jumapili, Griffiths alisisitiza kwamba watoaji misaada wamejitolea kuhakikisha wanawahudumia ipasavyo watu wenye mahitaji bila ya upendeleo. 


Griffiths alitilia mkazo haja ya kuhakikisha haki na usalama wa wanawake unalindwa, wakiwemo raia na watoaji misaada. Chini ya iliyokuwa utawala wa Taliban kati ya mwaka 1996-2001 nchini Afghanistan, haki za wanawake zilikiukwa zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...