Mji wa Kigali umeanzisha aina mpya ya kusafiri mjini humo kwa kutumia baiskeli kama sehemuyajuhudi za Rwandaza kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na kupunguza hewa ya kaboni katika miji na vituo vya miji vinavyoongezeka nchini humo.
Wasafiri wataweza kutumia baiskeli hizo kwa kupokezana katika mji mkuu Kigali kwa bei ya chini ikilinganishwa na usafiri mwingine uliopo mjini humo.
Mjini Kigali, mtaa wa Remera baiskeli nyingi zenye rangi ya kijani na manjano zimeegeshwa katika kila kona ya barabara.
Wakazi wa mji huo wanapakua application kwenye play store ya simu zao, ili waweze kutumia baiskeli yetu’’, anaeleza kijana wa kike ambaye amekuwa akitoa maelezo kwa wapita njia wanaoashuhudia jinsi ya matumizi ya maiskeli hizo.
Kuna vituo 13 vya baiskeli hizi mjini Kigali ambako pia kuna barabara maalumu za kuendeshea baiskeli. Mtaa wa Remera karibu na uwanja wa mpira kuna vituo vingine na baadhi wameanza kutumia baiskeli hizi.
Kwa mjibu wa kampuni ya ‘Gura Ride’ inayosimamia mpango huu anayetaka baiskeli anaichukua katika kituo kilicho karibuna kisha shughuli zake kuiweka kwenye kituo kingine kilicho karibu na mwisho wa safari yake.
Hatahivyo changamoto iliyopo bado nikwamba bado kuna barabara chache za kuendeshea baiskeli hizi mjini kigali ,pia milima iliyopo mjini Kigali inaweza kuwa kikwazo.
Lakini wahusika wana majibu kwa changamoto hizo, Jerry Ndayishimiye ni afisa wa GuraRide:
Meya wa jiji la Kigali Pudence Rubingisa amesema lengo kubwa la mradi huuni kukabiliana na uharibifu wa mazingira:‘’tunataka usafiri unaotusaidia kulinda uchafuzi wa mazingira, kusafiri bila kutumia magari kwani tutakaposafiri kwa kutumia baiskeli itakuwafaidakubwa kwa afya zetu kwa kupata hewa safi’’



No comments:
Post a Comment