Search This Blog

Wednesday, September 8, 2021

Mexico yahalalisha utoaji mimba katika uamuzi wa kihistoria


Mahakama ya juu zaidi nchini Mexico imeamua kwamba adhabu za kosa la jinai la kutoa mimba ni kinyume cha katiba.

Uamuzi huo uliotolewa katika jimbo la kaskazini la Coahuila, unazuia wanawake kushtakiwa kwa kutoa mimba.

Utoaji mimba kwa sasa umepigwa marufuku katika majimbo yote isipokuwa manne ya nchi hiyo.

Jaji wa mahakama ya juu zaidi Luis Maria Aguilar alielezea hatua hiyo kama "hatua ya kihistoria kwa haki za wanawake".

Siku ya Jumanne, mahakama iliamuru jimbo la Coahuila kuondoa vikwazo vya kutoa mimba kutoka kwa kanuni yake ya jinai.

Uamuzi huo unaweza kufungua njia ya kuruhusu utoaji mimba katika nchi nzima.

Hivi sasa, utoaji mimba ni halali tu katika majimbo machache, isipokuwa kwa visa vya ubakaji au ambapo maisha ya mama yako hatarini.

Chanzo cha mahakama kimesema uamuzi huo utaathiri Mexico yote, ikiruhusu wanawake katika majimbo ambayo utoaji mimba ni uhalifu kufanya utaratibu huo kwa agizo la jaji.

Kundi la Habari juu ya Chaguo la Uzazi (GIRE), ambalo linafanya kampeni za haki za utoaji mimba, lilielezea uamuzi huo kama "wa kihistoria"

"Tunatumahi kuwa kote nchini wanawake na watu wenye uwezo wa kubeba ujauzito wana hali na uhuru wa kuamua hatima yao ya uzazi", lilisema.

Coahuila inapakana na jimbo la Marekani la Texas, ambapo mahakama ya juu zaidi iliruhusu sheria ya serikali kupiga marufuku utoaji mimba wowote baada ya wiki sita za ujauzito.

Uamuzi huo unaweza kufungua njia kwa watu kutoka Texas wanaotaka huduma ya utoaji mimba halali.

 




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...