Kansela wa Ujerumani Angela Merkel yuko ziarani katika mji mkuu wa Poland Warsaw, kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki, wakati ambapo Poland inakabiliwa na shinikizo la uhamiaji Mashariki mwa mpaka wake na Belarus.
Serikali ya Poland imesema hii ni ziara ya mwisho ya kansela Merkel mjini humo na kwamba mazungumzo ya viongozi hao wawili, yatalenga pia kujadili namna ya kulinda mipaka ya nje katika mataifa ya Ulaya na janga la virusi vya corona.
Wawili hao pia watazungumzia uhusiano wa mataifa yao. Mkutano kati ya Merkel na rais Andrzej Duda, uliotangazwa awali na serikali ya Ujerumani hautafanyika.

No comments:
Post a Comment