
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amerudi nchini Ubelgiji ambapo amejiunga na mabingwa wa ligi hiyo Royal Antwerp kwa mkopo wa muda mrefu kutoka klabu ya fernabahce ya Uturuki.
Mchezaji huyo ametambulishwa rasmi hii leo katika tovuti ya klabu hiyo baada ya kutia saini mkataba wa muda usiojulikana
Kabla ya kujiunga na klabu hiyo mshambuliaji huyo alikuwa akiichezea klabu ya Uturuki ya Fernabahce ambayo alijiunga nayo kutoka klabu ya Uingereza ya Aston Villa.
Wakati alipojiunga na klabu hiyo ya Uturuki aliandikisha mkataba wa miaka minne.
Alijiunga na Aston Villa kutoka kwa Klabu ya Gent ya Ubelgiji
No comments:
Post a Comment