Search This Blog

Saturday, September 4, 2021

KIpa wa Yanga Farouk Shikalo asajiliwa KMC


FAROUK Shikalo aliyekuwa kipa namba mbili wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Septemba 4 ametambulishwa kuwa mali ya KMC.

Nyota huyo ambaye alikuwa anakipiga Yanga mkataba wake wa miaka miwili ulimeguka na mabosi wa timu hiyo waliamua kumuacha aende.

Hakuwa katika nafasi ya kudumu msimu uliopita kwa kuwa katika mechi 34 alikaa langoni kwenye mechi 10 za Ligi Kuu Bara. 

Aliweza kutwaa taji la Mapinduzi katika mchezo wa fainali uliochezwa Visiwani Zanzibar mbele ya Simba.

Anakwenda kuungana na kipa namba moja Tanzania, Juma Kaseja ambaye ni nahodha wa kikosi cha KMC ambacho kimeweka kambi Morogoro.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...