Search This Blog

Tuesday, September 7, 2021

Kim Kardashian ashutumiwa kuhamasisha sarafu ya matapeli mtandaoni


Kim Kardashian amekosolewa kwa kutangaza fedha ya kidigitali ambayo haijahalalishwa kwenye mtandao wake wa Instagram, na kiongozi wa mamlaka ya fedha nchini Uingereza.

Charles Randell amesema Bi. Kardashian aliwataka wafuasi wake mtandaoni ambao ni watu milioni 250, kubashiri tokeni ya kidigitali katika tangazo la Ethereum Max.

Bwana Randell ameuita kuwa ni ubashiri wa tokeni ya digitali iliyotengenezwa mwezi mmoja kabla ya waanzilishi wake ambao hawajulikani.

Na aliwashutumu washawishi kwa kuchochea "udanganyifu wa utajiri wa haraka"

Bwana Randell alikuwa anazungumza hayo katika kongamano la kimataifa la uhalifu wa kiuchumi.

Mwenyekiti huyo alisema ujumbe wa bi. Kardashian katika mtandao wa Instagram , ambao umewekwa kama tangazo , unaweza kupata uhamasishaji wa kifedha kwa wafuasi wengi wa mtu mmoja jambo ambalo ni historia.

Uhamasishaji wa tokeni inayofahamika kama Ethereum Max,alisisitiza kuwa usichanganywe nasarafu ya kidigitali ya Ethereum .

"Siwezi kusema kwa uhakika kuwa safari hii ni mbaya [Ethereum Max]," alisema.

"Lakini washawishi wa mtandaoni wamekuwa wakitumiwa na matapeli kuhamasisha sarafu mpya ambazo hazipo kabisa ," alisema.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...