Search This Blog

Tuesday, September 28, 2021

Jeshi nchini Guinea lazuia wanachama wake kushiriki uchaguzi mkuu ujao

Uongozi wa kijeshi nchini Guinea umewazuia wanachama wake kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao ambao hiyo itaashiria kurudi kwa utawala wa raia.

Hayo yanajiri wakati jeshi lilitangaza siku ya Jumatatu hati ya mpito ambayo ilimthibitisha kiongozi wa jeshi Kanali Mamady Doumbouya kama rais kufuatia mapinduzi ya mapema mwezi huu.

Hati hiyo pia inaangazia serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa raia na baraza la kitaifa la mpito ambalo litatumika kama bunge kwa muda.

Baraza hilo litakuwa na wanachama 81 kutoka kwa jamii na itajumuisha viongozi wa biashara ,vyama vya kisiasa, mashirika ya kidini, wanadiplomasia na mashirika ya kitaalamu. Pia wanazuiwa kushiriki uchaguzi wa ngazi ya mikoa na kitaifa.

Karibu asilimia 30 ya wanachama wa baraza hilo lazima wawe wanawake, na itajumuisha rais na makamu wake wawili .

Baraza litaamua juu ya urefu wa kipindi ambacho kitatawala kabla ya uchaguzi kufanywa ili kuanzisha serikali ya kidemokrasia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...