Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS imewawekea vikwazo vya safari na fedha, kikosi cha wanajeshi waliopindua serikali ya Guinea, pamoja na familia zao.
Uamuzi huo, umetangazwa baada ya kikao maalumu cha jumuia hiyo, kilichofanywa katika mji mkuu wa Ghana, Accra.
Vikwazo hivyo vinatarajiwa kuongeza shinikizo kwa wanajeshi hao kurejesha utawala wa Katiba.
Pia umoja huo unalitaka jeshi kufanya uchaguzi ndani ya miezi sita na kusisitiza kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayeruhusiwa kugombea katika uchaguzi huo.
Viongozi hao hata hivyo wameeleza utayari wao wa kuiunga mkono Guinea katika mchakato huo wa mpito
Wametoa wito kwa Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na washirika wao wa kimataifa kusaidia utekelezaji wa marufuku ya kusafiri na vikwazo vya fedha dhidi ya wanajeshi hao na familia zao.
Wanataka pia kutolewa bila masharti kwa Rais aliyeondolewa mamlakani Alpha Condé.

No comments:
Post a Comment