Search This Blog

Thursday, September 2, 2021

DCI Manumba kuzikwa leo Simiyu


Mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Tanzania (DCI), Robert Manunba utazikwa leo Alhamisi Septemba 2, 2021 nyumbani kwake Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu.

Manumba alifariki Agosti 30, 2021 majira ya saa 9 alasiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa maradhi ya figo ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amesema mazishi yatafuata taratibu zote za kijeshi.

"Alikuwa kiongozi wetu wa kijeshi kwa hiyo hata mazishi yake yatafanyika kwa kufuata taratibu za kijeshi chini ya Jeshi la Polisi," amesema Abwao.

Ameongeza kwamba jeshi limeandaa utaratibu wa kuwaongoza waombolezaji  watakaohudhuria katika mazishi hayo.

Manumba alijiunga na jeshi la Polisi 1976 na kulitumikia kwa miaka 37 hadi alipostaafu 2013.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...