Daktari maarufu wa Nigeria ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiudi kutoka kwenye mhadhara wa ukumbusho kwa heshima ya marehemu mke wake - afisa wa serikali aliyefahamika kwa kutibua njama ya wafanyabiashara wanaouza dawa bandia.
Dr Chike Akunyili alipigwa risasi usoni baada ya watu waliojihami kwa bunduki kushambulia gari lake katika mji wa Nkpor kusini mashariki mwa jimbo la Anambra, mwanawe wa kiume, Obumneme Akunyili, ameambia BBC Igbo.
Dereva wake na afisa wa polisi aliyekuwa akimlinda pia walifariki katika tukio hilo la ufyatulianaji risasi. Jamaa wake mmoja aliyenusurika kifo anapokea matibabu katika hospitali moja.
Walikuwa wakirejea nyumbani kutoka mji wa Nsukka uliopo jimbo la Enugu after baada ya kuhudhuria mhadhara ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Nigeria kwa heshima ya mke wa Dkt Akunyili, Dora Akunyili.
Wakati mmoja alikuwa mkuuu wa shirika la Nigeria la chakula na dawa, na aliheshimiwa sana kwa juhudi zake za kukabiliana na dawa bandia ambazo zilisambaa nchini Nigeria. Alifariki kutokana na saratani mnamo 2014.
Lengo la mauaji hayo haijulikani, lakini imewashtua Wanigeria wengi. Ni mauaji ya saba maarufu katika mkoa huo katika miezi nane iliyopita.
No comments:
Post a Comment