Mataifa ya Afrika yatapokea zaidi ya dozi milioni 100 za chanjo ya Covid zaidi ya kile wanachopokea kutoka mpango wa chanjo wa Covax kufikia mwishoni mwa mwaka, Shirika la afya duniani limesema.
Afrika ilikuwa inapokea dozi milioni 520 kufikia mwezi Disemba. Hivyo kwa upande wa Covax, wameweza kupata zaidi ya dozi milioni tano , kwa mujibu wa WHO.
Mpango wa Umoja wa mataifa wa kutaka dunia unasema mkataba wa pande zote mbili wa mataifa ambayo yanatengeneza ambayo yana mataifa tajiri pamoja na sheria za kudhibitisha zinalaumiwa kuwa sehemu ya kupunguza malengo yaliyowekwa.
Wakati chanjo ilipokuwa inasambazwa katika mataifa ya Afrika, angalizo lilitolewa na Covax kuwa hakuna dalili ya usawa jitihada za dunia za kutaka chanjo kutolewa kwa usawa bado haijazaa matunda.
Mataifa ya Afrika kwa kiwango kikubwa wanategemea Covax, lakini mpango huo wa Covax unashindwa kutoa chanjo kama ilivyohaidi.
Zaidi ya mataifa 54, ni mataifa 12 peke yake ndio yamefikia malengo ya dunia kwa kuwapa chanjo watu wake kwa 10% ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba.
Na taarifa kuwa baadhi ya mataifa tayari yameanza kupewa dozi za nyongeza licha ya wito kutolewa wa kutaka wasifanye hivyo mpaka mwishoni mwa mwaka, serikali za Afrika zinapaswa kufikiria namna ya kupata chanjo kwa ajili ya watu wake.
Ni asilimia 3% tu ya watu wa Afrika wamepata chanjo.

No comments:
Post a Comment