Search This Blog

Tuesday, September 7, 2021

Babake Britney Spears awasilisha rasmi ombi la kujiondoa kama msimamizi wa mali ya binti yake


Baba yake Britney Spears amewasilisha ombi katika mahamaka ya Los Angeles la kusitisha hadhi yake kama mtunzaji au msimamizi wa mali za binti yake aliyokuwa nayo kwa kipindi cha miaka 13 ambayo ilimpa fursa ya kusimamia maisha ya binti yake na fedha zake .

Jamie Spears aliandika kwamba binti yake "ana haki ya kufuatilia na kuhakikisha mahakama sasa inafikiria kwa uzito mkubwa ikiwa hadhi yake ya kumsimamia haihitajiki tena."

Britney Spears amekuwa akitafuta kumwondoa baba yake kwenye jukumu hilo mara mbili katika miaka miwili iliyopita.

Nyota huyo wa muziki aina ya pop ameelezea uhusiano wao kama "unyanyasaji" kiasi cha kukataa kufanya maonyesho chini ya usimamizi wa baba yake.

Hatua ya baba yake kuwasilisha ombi hilo mahakamani inawadia miezi miwili baada ya mwimbaji huyo kutoa ushahidi wa kushtusha mahakamani, akitaka hadhi ya kumtunza aliyo nayo baba yake kusitishwamara moja.

"Matukio ya hivi karibuni yanayohusiana na hadhi ya baba yake yametiliwa shaka ikiwa hali zimebadilika kiasi kwamba sababu za kuanzishwa kwake inawezekana hazipo tena" kulingana na ombi lililowasilishwa kwa mahakama kuu ya Los Angeles Jumanne.

"Bi Spears ameiambia mahakama kwamba anataka kudhibiti maisha yake mwenyewe bila ya msimamizi mtunzaji wake", ombi hilo linasema nakuongeza kuwa Spears ameelezea matumaini yake ya kujisimamia huduma zake za matibabu na kifedha.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...