KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuber Kabwe amepongeza juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuruhusu chanjo ya Ugonjwa wa Covid -19 kuingizzwa nchini na kutoa wito kwa Wanachama wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kupokea chanjo hizo.
Wito huo ameutoa leo Hayo wakati akifungua kikao maalumu cha dhararua cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Bait Yamini Mjini Unguja ambapo amesema kuwa amejiridhisha kuwa chanjo zilizoingia nchini ni salama na hazina madhara kwa wananchi hivyo ni wanachama wa Chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla wanatakiwa kujitokeza kupokea chanjo hizo.
Aidha Kiongozi huyo ametoa rai kwa viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuweka majadiliano ya Kitaifa yenye lengo la kujenga demokrasia ya Taifa.
Katika hatua Nyingine Zitto amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawaunganisha Watanzania pamoja kuendeleza mchakato wa katiba Mpya.
Katika kikao hicho cha Dharura cha Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kitajadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya Kiasa nchini na kuja maadhimio.

No comments:
Post a Comment