Search This Blog

Tuesday, August 10, 2021

Yanga yamtambulisha kipa mwingine


UONGOZI wa Yanga umemtambulisha nyota mpya ambaye ni kipa kutoka Aigel Noir.

Ni Erick Johola ambaye ni raia wa Tanzania na alionekana na Yanga katika siku ya Mwananchi.

Nyota huyo anakuwa ni kipa namba mbili baada ya kipa namba moja Diarra Djigui kutambulishwa ndani ya kikosi hicho na ni dili la miaka miwili ambalo amesaini.

Anakuja kuchukua nafasi ya Farouk Shikalo ambaye dili lake limeisha sawa na Metacha Mnata ambapo makipa hawa wote wawili hawajaongezewa kandarasi mpya.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...