Search This Blog

Sunday, August 8, 2021

Yanga yamsajili kipa kutoka Mali

 


RASMI hesabu za kumsajili kipa namba moja wa timu ya taifa ya Mali zimekamilika na atakuwa na timu hiyo msimu wa 2021/22.

Nyota huyo kutoka Mali, anaitwa Diarra Djigui ana umri wa miaka 26, na ni nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020.

Sababu kubwa ya Yanga kumpa dili kipa huyo ni kuwa chaguo namba moja la kocha wa Yanga, Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta kipa anayemtaka.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi kwa kuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia wanahitaji taji la ligi.

Usajili wa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Mali unatoa nafasi kwa Faroukh Shikalo kuchimba mazima Yanga.

Nyota huyo amepewa dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...