Search This Blog

Monday, August 30, 2021

Yanga yachezea kichapo siku ya Mwananchi


KIKOSI cha Yanga  kimepoteza katika mchezo wa kirafiki kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.

Alianza  Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...