Watu 8 waliuawa na 20 walijeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa mbele ya nyumba ya Waziri wa Ulinzi wa Afghanistan Bismillah Muhammedi katika mkoa wa Shir Pur wa Kabul jana jioni.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mirveyis Staniksey alisema katika taarifa kwa waandishi wa habari kwamba baada ya mmoja wa washambuliaji kulipua gari lililokuwa limesheheni bomu mbele ya nyumba ya Waziri wa Ulinzi Bismillah Muhammedi, washambuliaji wengine wanne waliingia kwenye nyumba nyingine na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Akieleza kuwa washambuliaji waliangamizwa usiku, Stanikzey alisema kuwa Waziri Muhammedi na familia yake hawakujeruhiwa katika shambulizi hilo.
Stanikzey pia alisema kuwa watu 8 walifariki katika shambulizi hilo, watu 20 walijeruhiwa, na raia kadhaa wanaoishi katika nyumba za eneo hilo walihamishwa.
Mashuhuda wa tukio walidai kwamba idadi ya watu waliokufa katika shambulizi ilikuwa zaidi ya 10.
Hakuna mtu ambaye amedai kuhusika na shambulizi hilo.
Mamlaka iliripoti kwamba maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka mikoa mingine walikuwa nyumbani kwa Mohammedi wakati wa shambulizi hilo.
Nyumba nyingi na sehemu za biashara karibu na nyumba ya Waziri pia ziliharibiwa na athari za bomu.
Baada ya shambulizi la bomu, raia wengi walilaani kitendo cha kigaidi huko Kabul.
Shir Pur, moja ya wilaya za kifahari zaidi za Kabul, ina nyumba za mawaziri na wabunge wengi.

No comments:
Post a Comment