Search This Blog

Sunday, August 22, 2021

Watoto zaidi ya 200 wenye ugonjwa wa Usonji kujengewa kituo Mwanza


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala amezindua mashindano ya mbio za Marathon leo hii mkoani Mwanza kwa lengo la kukusanya fedha ambazo zitasaidia kujenga kituo cha watoto wenye Usonji mbio hizo zinatarajia kufanyika tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka huu katika wilaya ya Nyamagana kata ya mkolani.


Zoezi hilo la mbio limeandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali Mwanza Charity run  kwa kushirikiana na Li-TAFO mara baada ya kubaini jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya ugonjwa wa Usonji. 

Masala amesema kuwa fedha ambazo zinatarajia kukusanywa katika zoezi hilo ni shilingi milioni mia tano zitajenga kituo ambacho kitawawezesha watoto hao aweze kupata huduma mbalimbali kama wapatazo wengine ili waweze kupata haki za msingi ambazo wanatakiwa kupatiwa  ikiwemo elimu,matibabu na michezo itakayo wajengea uwezo wa kutambua vitu.

Amesema katika ziara zangu nazo fanya katika kata swala  hili nitalifikisha na kuendelea kuielimisha jamii ambayo bado inadhana potofu juu ya watoto wenye ugonjwa wa Usonji na kuwanyanyapaa amesema Masala. 

Mkurugenzi wa Li-TAFO Muhandisi Shangwe Mgaya ameiomba jamii kutowaficha watoto wenye ugonjwa huo kwani wanahaki sawa kama watoto wengine Usonji siyo ushirikiana kama wangi wasemavyo na kupelekea kutoa kauli zisizofaa.

Amesema baadhi ya watu huwatuhumu wazazi wenye watoto wa Usonji kuwa wamewatoa kafara kutokana na muonekano wao katika familia na jamii amewasisitiza wanaume wenye tabia ya kukimbia familia inapotokea mke kazaa mtoto mwenye tatizo hilo bali washirikiane kumlea na kumpatia matibabu ili aweze kupata ufahamu ulio sahihi.

Mgaya ameongeza kuwa lengo la Taasisi hiyo ni kukusanya fedha katika mashindano hayo ambayo yatafanyika mwaka huu ili waweze kufikia lengo walilijiwekea kuweza kuwasaidia watoto wenye tatizo hilo amewaomba wadau mbalimbali wajitokeze kujiandikisha katika zoezi hilo la kukimbia mbio hizo ambalo linaanza tarehe 22 mwezi 8 katika viwanda vya Rock city more kwani watoto hao wanauhitaji matibabu ya ufahamu,kuongea na utambuzi wa vitu mbalimbali kutokana na gharama kuwa kubwa wanauhitaji msaada kutoka kwa jamii.

Naye katibu wa Mwanza Charity runners  Eid Zubery amewasisitiza wanamichezo wajitokeze katika zoezi hilo ambalo linania njema ya kuwasaidia watoto hao ikiwa ni zoezi la kwanza kufanyika mkoani hapa ili kuweza kujenga kituo kitakachowakusanya watoto hao ambao wanauhitaji maalum wa matibabu mbalimbali.


Amesema katika zoezi hilo la mbio Lina sehemu tatu ambazo ni kilometa 3kwa ajili ya watoto na wakubwa itakuwa ni kilometa 8 na kilometa 17  zoezi litafanyika kata ya Mkolani Nyahingi ambapo usajili umeishafunguliwa na lengo lao nikufanikiwa kupitia zoezi hilo ili kuwawezesha watoto zaidi ya 200 wenye uhitaji.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...