Search This Blog

Wednesday, August 11, 2021

“Wasanii mje Karimjee chanjo Uviko 19”- Dkt Abbasi

 Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeratibu zoezi la hiari kwa Wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya Covid19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya kazi zao wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Shime kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika”—Dkt. Abbasi

Abbas amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...