Search This Blog

Monday, August 30, 2021

UN inasema Korea Kaskazini inaonekana ikianzisha tena mitambo ya nyuklia


Inaelezwa kuwa Korea Kaskazini imeanzisha tena mtambo wake wa nuklia wa Yongbyon, Shirika la kiataifa la nguvu za atomiki la Umoja wa Mataifa limeeleza.

Plutonium, inayotuika kutengeneza silaha za nyuklia, inaaminika kuzalishwa katika mitambo hiyo.

Shirika la nguvu za atomiki (IAEA) lilifukuzwa na serikali ya Pyogyang waka 2009 lakini imekuwa ikitegemea picha za satelaiti ili kufanya tathimini.

Waangalizi wamesema mtambo huo umekuwa ukitoa maji baridi tangu Julai,wakidokeza kuwa ulikuwa ukifanya kazi.

Kinu cha Yongbyon,chenye mtambo wa megawatt-5, uko kwenye kitovu cha mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Hii ilikuwa ishara ya kwanza ya shughuli za kiutendaji katika kinu hicho tangu Desemba mwaka 2018, miezi kadhaa baada ya rais wa Marekani Donald Trump kukutana na Kim Jong-un huko Singapore, kwa mujibu wa IAEA.

Yongbyon kwa muda mrefu imekuwa ikifuatiliwa kutoka mbali na wataalam wanaojaribu kufahamu ni silaha ngapi utawala huo una uwezo wa kutengeneza.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...