Search This Blog

Saturday, August 21, 2021

Umoja wa Ulaya haulitambui kundi la Taliban

 


Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema umoja huo haulitambui kundi la Taliban na wala hautoshiriki mazungumzo ya kisiasa na kundi hilo. 


Von der Leyen ameyasema hayo wiki moja baada ya Taliban kuidhibiti Afghanistan ukiwemo mji mkuu Kabul. Aidha amesema atapendekeza Afghanistan iongezewe euro milioni 57 kwenye msaada wa kifedha ambao tayari umeshapitishwa na Umoja wa Ulaya, ili zisaidie kutoa misaada ya kiutu kwa raia wa nchi hiyo. 


Amesema msaada huo wa maendeleo unakwenda sambamba na kuheshimiwa kwa haki za binaadamu, kuwashughulikia vyema watoto walio chini ya miaka 18 na kuheshimu haki za wanawake na wasichana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...