Search This Blog

Sunday, August 22, 2021

Tutaimarika zaidi, Tutakuwa tofauti - Didier Gomes

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes, amesema kuwa anawaamini wachezaji wake na anajua kwamba watakuwa tofauti  kwa msimu ujao kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.

Wakiwa nchini Morocco,  jana Agosti 21 walicheza mchezo wa kirafiki na FAR Rabat na ngoma kukamilika 2-2 jambo ambalo limemfurahisha kocha huyo.


Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kucheza tangu walipoweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.

Gomes amesema:"Nafurahishwa na namna ambavyo wachezaji wangu wamafanya ni furaha kwangu na kwao pia. Kwa hali ilivyo nadhani tutazidi kuwa bora zaidi.

"Bado tuna mwezi mmoja wa kufanya kazi na maandalizi zaidi hivyo bado tuna muda wa kujiaandaa kwa ajili ya msimu ujao na ninafurahishwa na kile ambacho wachezaji wanakifanya,".

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...