Manchester City inatayarisha dau la £150m kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, huku vyanzo vikisema kwamba kitita hicho huenda kikatosha kuishawishi Tottenham na mwenyekiti wake Daniel Levy kuanza mazungumzo. (Independent - subscription required)

Ikiwa Manchester City itashindwa kumpata Kane msimu huu, inasemekana mabingwa hao wa Ligi ya Primia wanafikiria kumchukua mchezaji wa kimataifa wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, kama mbadala wake. City imeripotiwa kujiunga na wengine wanaomsaka mshambuliaji wa Fiorentina kwa euro milioni 80. (Firenze Viola - in Italian)

Liverpool imepata pigo katika mbio zake za kumsaka Mreno kiungo wa kati wa Lille Renato Sanches, 24, ambaye huenda akakosa mechi kwa wiki 6 kwasababu ya jeraha. (Mirror)

Arsenal huenda iko tayari kwa makubaliano ya mabadilishano yatakayogharimu kima cha £34m kumpata mchezaji wa Real Madrid raia wa Uhispania, 25, Marco Asensio. (Fichajes - in Spanish)

Tottenham imeimarisha nia yake ya kumsaka mlinzi wa Fiorentina raia wa Serbia Nikola Milenkovic baada ya West Ham kuamua kutomfuatilia mchezaji huyo, 23. (The Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 29, huenda akafikia mkataba wa muda mrefu na Liverpool. (Times)

Newcastle imeweka kiwango cha dau la £10m kumuuza kiungo wa kati Sean Longstaff. Mkataba wa mchezaji huyo, 23, huko St James' Park unafikia ukomo wake msimu ujao na kocha wa Everton Rafa Benitez inasemekana kwamba anafikiria kufanya mazungumzo ya kumchukua na kumpeleka Goodison Park. (Mail)

Arsenal na Manchester United zimeombwa kusahau kuhusu suala la kumsajili beki wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 30. (AS)

Everton huenda ikamsajili mshambuliaji wa Schalke Matthew Hoppe kwa dau la chini ya £7m thamani ya Mmarekani huyo kwasababu ya hali ya kifedha ya klabu hiyo ya Ujerumani. Toffees ni moja ya timu kadhaa zenye nia ya kumsajili mchezaji huyo, 20, kwa kitita cha £4m na bado itachukuliwa kama makubaliano mazuri ya kibiashara. (Bild - in German)

Liverpool iko "kifua mbele" kwa wanaowania kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21. (Sport1 via Sport1 via Mirror)

Dau la Crystal Palace la £5m kwa kiungo wa kati Will Hughes, 26, limekataliwa na Watford. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 32, amerejea Real Madrid baada ya kuunganishwa na Carlo Ancelotti, kutokana na kutofautiana na Zinedine Zidane hapo awali. (Marca - in Spanish)

Leeds United imefanya majaribio kadhaa kumsajili beki wa kushoto wa Celtic raia wa Scotland Matthew Anderson, 17, msimu huu lakini dau lake limekataliwa. Klabu hiyo bado inafikiria makubaliano ya kumleta mchezaji mwenza Anderson kutoka timu ya Celtic, mlinzi wa Norway Leo Hjelde, 17, kwenda Elland Road.(Yorkshire Evening Post)

Juventus imeshindwa na Liverpool na Tottenham kumsajili Mbrazil Kaio Jorge, 19, Santos. (Goal)

Manchester United bado inafikiria uwezekano wa kumsajili kiungo mwingine wa kati. Makubaliano yoyote yale yatahitaji kufadhiliwa na kuondoka kwa mchezaji kwasababu ya kuchukuliwa kwa beki wa kati raia wa Ufaransa Raphael Varane, 28, na winga wa England Jadon Sancho, 21. (Manchester Evening News)

Aliyekuwa nyota wa Newcastle na Chelsea Demba Ba, 36, ameondoka Lugano ya Uswizi, huku mchezaji huyo wa Senegal akichezea klabu hiyo dakika 48. (talkSPORT)

Barcelona ina matumaini ya kutafuta euro milioni 200 kupunguza deni lake kupitia kumuuza raia wa Ufaransa, 27, Samuel Umtiti, nyota wa Brazil Philippe Coutinho, 29, na mchezaji wa Bosnian Miralem Pjanic, 31. (Goal)

Kiungo wa kati wa Arsenal Joe Willock, 21, anatarajia kuvunja rekodi ya Alan Shearer ya kufunga magoli mfululizo na kuweka historia katika kujitokeza kwa mara ya pili kupitia timu ya Newcastle dhidi ya Aston Villa wikendi hii. (Mirror)