Search This Blog

Tuesday, August 10, 2021

Taliban wadhibiti mji mwingine nchini Afghanistan

 Wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa mji mkuu mwingine wa mkoa wa kaskazini mwa Afghanistan. Huo ni mji mkuu wa sita wa mkoa kuangukia mikononi mwa Taliban katika kipindi cha siku nne zilizopita. 


Kulingana na diwani Raz Mohammad na wabunge wawili wanaoliwakilisha jimbo hilo, kundi hilo la waasi limeteka vituo vikuu vya serikali katika mji wa Aybak ambao ni mji mkuu wa jimbo la Samangan. Vikosi vinavyoiunga mkono serikali viliuacha mji huo na kukimbilia kwenye kilima cha Koh-e Bast baada ya serikali kuu kushindwa kupeleka nyongeza ya askari na haikutekeleza mashambulizi ya angani kuvisaidia vikosi vya serikali. 


Hata hivyo mbunge mwingine kutoka kwenye eneo bunge hilo amesema askari wengine wapya 300 watapelekwa ili kusaidia operesheni ya kuwashinikiza Taliban kuondoka kutoka kwne mji wa Aybak, wenye wakazi zaidi ya 120,000. 



Hapo jana wanamgambo wa Taliban waliiteka miji mikuu mitatu ya Kunduz, Sar-e Pul na Taluqan. Wapiganaji wa Taliban wamechukua zaidi ya nusu ya wilaya za Afghanistan wakati ambapo majeshi ya Marekani na NATO yanakamilisha hatua za kuondoka kabisa nchini humo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...