Search This Blog

Thursday, August 26, 2021

Spishi mpya ya nyangumi wa kale wenye miguu minne yagunduliwa Misri



Wanasayansi huko Misri wamegundua spishi mpya ya nyangumi wenye miguu minne ambao waliishi karibu miaka milioni 43 iliyopita.

Mabaki ya spishi hiyo kwa jina Phiomicetus anubis awali yaligunduliwa katika Jangwa la Magharibi la Misri.

Fuvu la kichwa chake linafanana na Anubis, mungu wa zamani wa mbwa-mwitu wa Misri wa wafu ambaye aliitwa jina lake.

Kizazi cha kale cha nyangumi wa kisasa walitengenezwa kutoka kwa wanyama kama kulungu ambao waliishi ardhini kwa kipindi cha miaka milioni 10.

Akiwa na uzani wa kilo 600 na mita tatu (10ft) kwa urefu, Phiomicetus alikuwa na taya kubwa na ngumu ili kuwakamata mawindo, kulingana na utafiti uliochapishwa na Proceedings of the Royal Society B Jumatano. Nyangumi huyo aliweza kutembea ardhi na kuogelea ndani ya maji.

Mifupa ya sehemu yake ilipatikana katika Fayum Depression nchini Misri na kuchambuliwa na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Mansoura. Ingawa eneo hilo sasa ni jangwa, wakati mmoja lilikuwa limefunikwa na bahari.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...