Search This Blog

Friday, August 6, 2021

Samaki mwenye meno ya binadamu avuliwa Marekani


Samaki asiye wa kawaida mwenye meno ya binadamu amevuliwa nchini Marekani, picha ya samaki huyo ilisambazwa katika mtandao wa facebook .

Alitambuliwa kama samaki mwenye kichwa cha kondoo {Sheephead fish}, ambaye ana meno kama ya binadamu ya kuvunja chakula.

Samaki huyo anaonekana kupata jina hilo kutokana na mdomo wake kuwa na muonekano kama ule wa kondoo.

Samaki huyo anadaiwa alikamatwa na Nathan Martin ambaye amekuwa katika gati hiyo.

Bwana Martin alisema alikuwa na matumaini ya kumshika samaki mwenye kichwa cha kondoo wakati alipoona mdomo uliojaa meno.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...