Rais Cyril Ramaphosa jana Alhamis amewataja mawaziri wapya wa afya, ulinzi na fedha, ikiwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya baraza lake la mawaziri baada ya machafuko makubwa yalisababisha na hukumu ya kifungo cha mtangulizi wake Jacob Zuma.
Amembadilisha waziri wa afya wa taifa hilo, Zweli Mkhize, ambae kwa kiasi kikubwa anaheshimika kwa namna alivyolishughulikia janga la virusi vya corona, lakini ambae pia ana kashfa ya ufisadi kuhusu fedha za ufadhili kwa ajili ya janga hilo.
Nafasi yake imechukuliwa na Joe Phaahla, ambae hadi wakati huu ni naibu waziri wa afya. Ramaphosa amebadili mawaziri 10, katika kipindi cha majuma kadhaa tu, jambo ambalo mwenyewe analitetea kwa kusema mabadiliko ya mawaziri ni muhimu pale inapotekea changamoto.

No comments:
Post a Comment