
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewaambia maafisa wanaosimamia mifumo ya haki kuhusu tatizo sugu la rushwa kwenye mfumo wa mahakama na anasema hayo kuwakilisha kilo cha wananchi wake.
Akizungumza na maafisa wa ngazi za juu kutoka wizara ya sheria mjini Bujumbura siku ya Jumanne, Rais Ndayishimiye alisema, amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka nchi nzima kuhusu usimamizi mbovu wa haki na utendaji kutokana na rushwa.
“Hamnionei huruma ninavyolia mbele yenu? aliuliza rais huyo kwa sauti ya hisia.
Rais huyo alisema rushwa imesababisha maelfu ya kesi ziwekwe kando bila kutolewa maamuzi kwa miaka mingi.
Alisema kiwango cha rushwa kwenye mifumo ya haki ya nchi hiyo inazuia mpaka wakewekezaji kwenda Burundi kuwekeza kwa sababu hawawezi kwenda kwenye nchi ambayo hawawezi kupata haki.
Maoni na maneno hayo ya Rais Ndayishimiye yanathibitisha maneno ya mashirika ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya nchi hiyo, yaliyokuwa yanasisitiza kuwa rekodi mbaya ya haki za binadamu nchini humo ni sehemu ya matokeo ya mfumo wa mahakama uliojaa rushwa.
Hata hivyo huenda asiwashawishi watu wengi ambao wanaamini kwamba taasisi yake inapaswa kuwajibika katika nchi ambayo muhimili wa serikali umepewa nguvu zaidi.
No comments:
Post a Comment