Search This Blog

Friday, August 20, 2021

Rais wa Afghanistan: ''Niliihama nchi ili kuzuia umwagikaji wa damu


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani alisema kuwa aliihama nchi yake ili kuzuia umwagikaji wa damu.

Ashraf Ghani alikosolewa vikali na mawaziri wa zamani kwa kuondoka ghafla nchini wakati vikosi vya Taliban viliingia mji mkuu wa Kabul siku ya Jumapili.

Ghani, ambaye jana alitangazwa kuwa katika Falme za Kiarabu, alitoa taarifa kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka nchini.

Katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video na kuchapisha kwenye akaunti yake ya Facebook, Ghani alisema kwamba ilimbidi aondoke Afghanistan ili kuzuia umwagikaji wa damu na maafa makubwa kutokea.

Ghani pia alikanusha ripoti kwamba alichukua pesa nyingi wakati alipoondoka ikulu ya rais.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...