Search This Blog

Tuesday, August 10, 2021

Rais mpya wa Iran ampigia simu Macron kuhusu mazungumzo yaliyokwama ya nyuklia

 Rais mpya wa Iran Ebrahim Raisi amemhimiza mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kusaidia kuzilinda haki za Iran katika mazungumzo ambayo sasa yamekwama ya kuufufua muafaka wa nyuklia wa Iran na mataifa yenye nguvu duniani. 

Katika mazungumzo yake ya kwanza ya simu na kiongozi wa Magharibi, Raisi, aliye na msimamo mkali na ambaye alichukua madaraka wiki iliyopita, alimwambia Macron kuwa Marekani na Umoja wa Ulaya lazima zitekeleze ahadi zao chini ya muafaka wa kihistoria wa 2015. 

 Ufaransa, pamoja na Marekani, Ujerumani, Uingereza, Urusi na China ilikuwa sehemu ya makubaliano ya awali ya nyuklia mnamo mwaka wa 2015 na imekuwa na jukumu kubwa kama mpatanishi. 

Rais amesema katika mazungumzo yoyote, haki za taifa la Iran zinapaswa kulindwa, huku akiikosoa Marekani kwa kujiondoa katika makubaliano hayo na kutangaza vikwazo vipya chini ya Rais wa zamani Donald Trump.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...