Search This Blog

Sunday, August 29, 2021

Prof. Shemdoe afanya msawazo wa Wahandisi, Wasanifu na Wakadiriaji Majengo

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe  amesema kuna uhaba wa Wahandishi katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kitu ambacho kinapelekea miradi ya ujenzi inayotekelezwa kupitia Force account kuzorota.

Akifafanua kauli hiyo akiwa ziarani Manispaa ya Kahama wakati akijibu swali la Mkurugenzi wa Kahama kuhusu kukosekana kwa Mhandisi katika Halmashauri hiyo amesema kuna Sekretariet za Mikoa 11 kati ya 26 zilizopo Nchini ambazo hazina Mhandisi hata mmoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa 53  hazina Mhandisi kabisa.

Pia Prof. Shemdoe amesema kuna baadhi ya Halmashauri zenye mhandishi zaidi ya mmoja. 

‘Kulingana na hali hiyo nimeona ni vyema Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufanya msawazo wa Wahandisi kwa kuhamisha Wakuu wa Idara za Ujenzi 10 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda katika Sekretarieti za Mikoa kwa ajili ya kufikiriwa kujaza nafasi za Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu;  amesema

Aliongeza kuwa Wahandisi 3 kutoka Sekretarieti za Mikoa wamependekezwa  kuhamishiwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi na Wahandisi 21 kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wamependekezwa kuhamishiwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nyinginezo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi

Prof. Shemdoe alihitimisha kuwa Wakadiriaji Majengo na Wasanifu Majengo 32 kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye Wahandisi watahamishiwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo hazina Wahandisi.

Msawazo  huu sasa utasaidia kuhakikisha miradi mingi ya majenzi inayoendelea huko Kwenye Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambako Serikali imepeleka na inaendelea kupeleka  fedha kwa wingi itasimamiwa kwa ubora zaidi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...