
Polisi nchini Ghana imeufahamisha umma kuwa wataendesha maziko ya miili ya watu 200 ambao hawajatambuliwa na jamaa zao.
Miili hiyo itaanza kuzikwa mwishoni mwa wiki hii, kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi la nchi hiyo.
Ofisa mmoja wa Polisi ameiambia BBC kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa maiti kwenye hospitali za jeshi hilo.
Miili hiyo ni ile iliyokusanywa katika kipindi cha miezi sita iliyopita na ni ya watu waliopata ajali na watu masikini ambao walifariki mitaani, alisema ofisa wa Hospitali moja ya jeshi la Polisi Ghana.
Ameongeza kuwa ipo miili ya watu waliohusika kwenye makosa ya jinai na wengine walifariki walipokuwa wamelazwa Hospitalini na kutelekezwa na ndugu zao.
Polisi imewataka wananachi kuwasiliana na kitengo chao cha Patholojia ili kutambua miili hiyo.
Ni kawaida kwa Hospitali za Polisi nchini humo kufanya maziko ya aina hiyo kwa miili isiyotambuliwa , licha ya kwamba shughuli za maziko ni utamaduni muhimu kwa Waafrika.
No comments:
Post a Comment