Search This Blog

Thursday, August 26, 2021

Nigeria:Watu waliojihami wawaachilia watoto wa shule waliokuwa wakishikiliwamateka


Wapiganaji wenye silaha nchini Nigeria wamewaachilia huru wanafunzi waliotekwa nyara kutoka shule moja ya Kiislamu mnamo Mei, kulingana na mwalimu wao mkuu.

Wanafunzi 136 kutoka shule hiyo huko Tegina, jimbo la Niger, walikamatwa na watu wenye silaha wakidai fidia.

Maafisa wa shule wanasema wanafunzi 15 walitoroka mnamo Juni na wengine sita walifariki wakiwa mateka

Utekaji nyara wa watu wengi kwa ajili ya fidia umekuwa jambo la kawaida nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni.

Mwalimu mkuu Abubakar Alhassan alisema hangeweza kutoa idadi kamili ya wanafunzi walioachiliwa, lakini "hakuna mwanafunzi aliye aliyeshikiliwa mateka ".

Aliliambia shirika la habari la AFP kwamba wanafunzi hao walikuwa wakisafirishwa kwenda nyumbani.

Bado haijafahamika jinsi wanafunzi hao walivyoachiliwa.

Fati Abdullahi, ambaye binti wakemwenye umri wa miaka 18 na mtoto wake wa kiume wa miaka 15 walichukuliwa na kikundi hicho, alisema watoto wake walikuwa wameachiliwa.

"Tunatamani kuwaona," alisema.

Mnamo Mei 30, watu wenye silaha waliokuwa wakitumia pikipiki walivamia mji huo na kufyatuarisasi huku wakimuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine.

Watu walipokimbia, washambuliaji walikwenda shuleni na kuwakamata watoto hao.

Mnamo Julai, watekaji nyara walimkamata mtu ambaye alitumwa kupeleka malipo ya fidia ili kuhakikisha kuachiliwa kwa wanafunzi.

Wazazi na wasimamizi wa shule walikuwa wameuza mali na sehemu ya ardhi ya shule hiyo kulipa fidia. Lakini baadaye walisema malipo hayakutosha .

Zaidi ya wanafunzi 1,000 wametekwa nyara kutoka shule kaskazini mwa Nigeria tangu Disemba mwaka jana.

Mamlaka huko zimekosolewa kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini kote ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...