Mahakama ya China imemuhukumu mfanyabiashara kutoka Canada kwa kosa la ujasusi na kumpa kifungo cha miaka 11 gerezani.
Michael Spavor alikuwa ameshikiliwa tangu mwaka 2018, baada ya kukamatwa na mwanadiplomasia wa zamani wa Canada Michael Kovrig.
Hukumu hiyo inaweza kuleta mvutano wa mahusiano kati ya serikali ya Canada na China.
Hii inakuja kama vita vya mapambano ambayo hayajazoeleka yanayomuhusisha Meng Wanzhou, Mkurugenzi mkuu wa kampuni kubwa ya simu Huawei, yaliyotokea Canada.
Wakosoaji wameishutumu China kwa kuwahusisha Spavor na Kovrig kwa kuwaweka mateka wa diplomasia.
Katika taarifa iliyochapishwa Jumatano, mahakama ya Dandong ilisema: "Kwa uhalifu wa upelelezi na utoaji wa siri nje ya nchi kinyume na sheria [Spavor] amehukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani , kulipa yuan 50,000 ($7715: £5578) thamani ya mali zake binafsi na kufukuzwa."
Hata hivyo, taarifa hiyo haikuweka wazi ni lini uhamisho huo utafanyika lakini China kawaida huwahamisha wageni waliopatikana na hatia baada tu ya kumaliza kifungo chao gerezani.
Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema hukumu hiyo haikuwa ya haki kabisa na haikubaliki.
Hukumu hiyo imekuja miaka miwili na nusu baada ya kushikiliwa huku kukiwa hakuna uwazi katika hatua za kisheria na hata kufikia kiwango cha chini cha sheria za kimataifa, kwa mujibu wa ripoti ya Reuters ameeleza.

No comments:
Post a Comment