Search This Blog

Monday, August 9, 2021

Maulid Kitenge afunguka kuhusu akaunti yake ya insragram kudukuliwa

 

 Kufuatia sintofahamu juu ya akaunti za MtangazajiMaulid Kitenge baada ya kuwa hazipatikani hapa Instagram, leo ameweka wazi kuwa akaunti hizo zimedukuliwa.

Akizungumza na mtangazaji Gerald Hando Asubuhi hii kwenye kipindi cha "Joto Kali la Asubuhi" cha EFM amesema baada ya kuanza mchakato wa kurudi kwenye kituo chake hicho cha awali (EFM) akaunti zake mbili za instagram zilidukuliwa.

#Maulid ameeleza kuwa hajatendewa haki kwani akaunti hizo ni sehemu nyingine anayotumia kupata riziki, na hajui ni nani amefanya kitendo hicho, anasikia watu wengi wakihisi watu lakini yeye hajui ni nani amefanya hivyo.

Mtangazaji huyo nguli wa Habari za Michezo nchini, amemalizia kwa kusema kwasasa hana akaunti Instagram, ametoa ahadi kuwa akaunti hizo zitarudi.

Ikumbukwe #MaulidKitenge 'Chumvi' amerudi EFM baada ya kuachana na kituo cha redio cha WasafiFm alichokuwa anafanyia kazi. Alitangazwa rasmi kurejea EFM Agosti 6, na Mkurugenzi wa TVE na redio EFM, Francis Ciza maarufu @majizzo alimkaribisha #Maulid kurejea kituoni hapo akisema kwamba amerudi NYUMBANI.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...