Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imeongeza wanachama watano waandamizi wa makundi ya itikadi kali barani Afrika kwenye orodha yake mbaya ya ugaidi, huku ikizuia mali zao na maslahi yoyote waliyo nayo nchini Marekani.
Wa kwanza kuongezwa kwenye orodha hiyo ni Bonomade Machude Omar, kamanda mwandamizi wa kundi la Dola la Kiislamu - IS nchini Msumbuji, aliyeongoza shambulizi kali kwenye hoteli ya Amarula mjini Palma mwezi Machi.
Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken imesema Omar pia alihusika na mashambulizi mengine nchini Msumbiji na Tanzania.
Wengine waliowekwa kwenye orodha hiyo ni Sidan ag Hitta na Salem ould Breihmarr, viongozi waandamizi wa tawi la Al-Qaeda nchini Mali la Jama'at Nasr al-Islam wal Muslimin - JNIM. Ali Mohamed Rage, msemaji wa kundi la al-Shabaab, na Abdikadir Mohamed Abdikadir, anayesimamia mipango ya operesheni za kundi hilo, pia wamejumuishwa.

No comments:
Post a Comment