Marekani imetoa tahadhari nyingine ya usalama kwa raia wake nchini Afghanistan.
Katika taarifa ya tahadhari uliotolewa kwenye wavuti ya Ubalozi wa Marekani huko Kabul, iliandikwa,
"Raia wa Marekani wanapaswa kuepuka kusafiri kwenda uwanja wa ndege wakati huu na kukaa mbali na milango ya uwanja wa ndege."
Taarifa hiyo pia ilijumuisha onyo kwamba "raia wa Marekani katika Lango la Abbey, Lango la Mashariki au Lango la Kaskazini wanapaswa kuondoka mara moja."

No comments:
Post a Comment