Search This Blog

Thursday, August 26, 2021

Makamu wa Rais wa Marekani asisitiza shinikizo zaidi dhidi ya China


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alisema kuwa watapata njia mpya za kuongeza shinikizo kwa China.

Katika ziara yake huko Vietnam kusisitiza kujitolea kwa Marekani katika bara la Asia, Harris alikutana na Rais Nguyen Xuan Phuc.

Katika mkutano huo, Harris alisema kuwa Marekani itaendelea kupinga ubabe wa Beijing katika Bahari ya Kusini mwa China,

"Lazima tutafute njia za kushinikiza Beijing kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Sheria ya Bahari na kuongeza shinikizo," alitoa maelezo hayo.

Alipokuwa Singapore kwenye ziara yake ya kikanda, Harris alieleza kuwa Marekani ingeunga mkono washirika wake katika eneo hilo dhidi ya vitendo vya China, akisema kwamba vitendo vya China katika Bahari ya Kusini mwa China vinahusiha "shinikizo" na "vitisho".

China, kwa upande mwingine, iliishutumu Marekani kwa kuwa mnafiki na kujaribu "kulazimisha na kutisha" nchi katika eneo ndani ya "mpango wao wa kuchukua udhibiti wa China".

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...