Search This Blog
Thursday, August 26, 2021
Majeruhi wa tukio la shambulio la silaha wafanyiwa upasuaji, wawili waruhusiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea majeruhi watano jana tarehe 25 Agosti, 2021, kuanzia majira ya saa saba mchana wakiwa na majeraha makubwa na wengine madogo sehemu mbalimbali za miili yao ambapo wanne kati yao ni Askari wa Jeshi la Polisi na mmoja ni Mlinzi wa kampuni binafsi ya SGA.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya umma Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema, Mara tu baada ya kupokelewa, askari wawili ( miaka 41 & miaka 49) walikua na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za Mwili na ya viungo vya ndani hivyo kufanyiwa upasuaji wa haraka ambapo upasuaji ulienda vizuri.
Askari wa tatu (miaka 35) naye alipata majeraha mbalimbali makubwa na madogo katika maeneo ya mikono na mgongoni ambaye alipewa huduma stahiki na kufungwa vidonda.
Askari wa nne (miaka 46), alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani kwakua alikua na majeraha madogo.
Mlinzi wa SGA (miaka 42) naye alikuwa na majeraha ambayo hayakuhitaji upasuaji hata hivyo alilazwa wodini jana na ameruhusiwa leo kwenda nyumbani kuendelea na matibabu akiwa nyumbani
Hivyo, tumebakiwa na majeruhi watatu ambao wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.
Hata hivyo tulipokea mwili wa marehemu mmoja kutoka kwenye tukio hilo ambaye alikuwa ni Mlinzi wa SGA na mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment